• Cate Waruguru alichaguliwa kuwa mwakilishi wa wanawake kaunti ya Laikipia kwa tiketi ya chama cha Jubilee katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017
  • Waruguru alikuwa akifanya kazi kwa karibu na naibu Rais William Ruto chini ya kikundi cha Tanga Tanga kabla ya kuhamia kikundi cha Kieleweke kinachohusishwa na Rais
  • Mbunge huyo ameelezea kutoridhishwa na uongozi wa chama hicho na sasa amesema anapanga kukihama

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Laikipia Cate Waruguru amedokeza kwamba huenda akakihama chama cha Jubilee kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022 kufika.

Habari Nyingine: "Wacha Kukopi Embarambamba" Wakenya Wamkemea Mwimbaji Geoffrey Magembe

Habari Nyingine: Sharon Otieno: Maafisa wa DCI Walishindwa Kuchukua Alama za Vidole Kwenye Vitu Waliokota Eneo la Mauaji

Akizungumza akiwa kwenye mahojiano na runinga ya KTN Jumatano, Julai 14, Waruguru alisema kuna utata mkubwa katika chama hicho na ameonelea ni vema kujiondoa kabla mambo kuharibika zaidi.

Waruguru alisema kumekuwa na mvutano na matatizo mengi licha ya viongozi wakuu kushinikiza kutafuta suluhu ili kukifufua chama.

Pia soma

Kariri Njama na Njuguna Wanjiku Wapiga Kura, Kusubiri Kujua Aliyechezwa na Wakazi

"Wanachama wengi wamekihama chama cha Jubilee, hivi karibuni nami pia nitatangaza uamuzi na msimamo wangu," Waguru alisema.

Habari Nyingine: Mwanafunzi wa Maseno School Aaga Dunia Baada ya Kuumwa na Kichwa

Hata hivyo, Waruguru hakufichua anakoelekea lakini alisema atafanya mazungumzo na wakazi wa Laikipia waliomchagua kuwakilisha kwanza kabla ya kufanya uamuzi.

" Nitafanya uamuzi wangu hivi karibuni baada ya kufanya mazungumzo na bosi wangu ambao ni wakazi wa Laikipia," Aliongezea Waruguru.

Waruguru alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa Wanawake kaunti ya Laikipia kwa tiketi ya chama cha Jubilee katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.

Wakati siasa za Tanga Tanga na Kieleweke zilipoanza, aliungana na naibu Rais William Ruto ndani ya kikundi cha Tanga Tanga kabla kuhamia Kieleweke kinachohusishwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Madai ya Waruguru yanajiri takribani mwezi mmoja baada ya mwakilishi wa wanawake wa Kiambu Gathoni Wa Muchomba kuhamia mrengo wa DP Ruto.

Wa Muchomba alijiunga na Tanga Tanga siku ya Jumatano, Juni 23 ambapo alifanya mkutano na Naibu Rais nyumbani kwake mtaani Karen.

Pia soma

Uchaguzi Kiambaa: Vijana Wamzomea Amos Kimunya Wakidai Anataka Kubadilisha Kura

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoV5hZhmpLCZm565qr%2FHomSwmV2srq%2Bt1pqinmWclrastc%2BimGabkamybsPAq6ygraKqeqKwzqScs5ldoMKstceapJplk52urq2MnJ%2BaZZqqr6q4xJ5loaydoQ%3D%3D