- Kevin na wenzake walicharazwa vilivyo na baadaye kufukuzwa kwa kutohudhuria masomo darasani
- Alipata majeraha mabaya sana mguuni baada ya kupigwa na mjeledi wa mpira
- Mama yake Kevin sasa annawataka polisi na wizara ya elimu kuingilia kati
Mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Upili la Gitongu ya Mathioya, Kaunti ya Muranga amelazwa katika Hospitali ya Muranga Level Four baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya na walimu watano wa shule yake.
Kevin Maina, 17 alipata majeraha kwenye mguu wake wa kulia kufuatia mijeledi ya mpira aliyolishwa na walimu hao wa kiume.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Mwanamuziki chipukizi wa Kikalenjin - Msupa S - amepoteza njia? Video yake yasisimua Wakenya

Akizungumza akiwa kitandani alikolazwa, Kevin alisema masaibu yake yalianza kabla ya shule kufungwa kwa likizo ya Aprili.
Anasema hawakuwahi shuleni kwa sababu mtihani uliokuwa ukiendelea haukuwa wao, lakini waliitwa siku iliyofuatia kusema ni kwa nini hawakuwa shuleni.
Habari Nyingine: Binti avaa 'nusu uchi' akiuza maji barabarani, watu wazua mjadala mitandaoni

“Ofisi naibu mwalimu mkuu, Njaramba aliungana na walimu wengine wanne ambao walitutandika na mijeledi ya mipira migongoni, makalioni na sehemu nyinginezo," alisimulia.
"Mmoja wa mjeledi wa mwalimu Njaramba ulinipata ndani ya paja la mguu wangu wa kulia,” Maina aliiambia TUKO.co.ke huku akitiririkwa na machozi.
Baadaye yeye na wenzake walitimuliwa shuleni na hali ya mguu wake ikaanza kuwa mbaya na kumlazimu mama yake kutafuta matibabu.
Habari Nyingine: Vera Sidika arekodi video ya shabiki wake wa kiume aliyemuacha hoi, amuahidi zawadi

"Nimepasuliwa mara mbili kutoa usaha na maji kutoka katika kidonda hiki na nahisi uchungu mwingi sana,” Kevin aliiambia Tuko.co.ke.
Mama ya Kevin, Lucy Wanjiku amewalaumu walimu kwa kumpiga mwanawe na kumuumiza kinyume na kanuni za shuleni.
“Walimu walisema sina pa kuwapeleka, mwalimu mkuu aliniambia nisifuatilie suala hilo kituo cha polisi, vyombo vya habari ama maafisa wa elimu na kuahidi kulipia gharama za hospitalini," alisema.
Habari Nyingine: Je, Rick Ross alilala kitanda kimoja na Mwalimu Rachael wakati wa 'concert' yake Nairobi?
Sasa anawataka polisi na wizara ya elimu kuliingilia suala hilo ili walimu husika kuchukuliwa hatua na kuwajibishwa.
TUKO.co.ke iliitembelea shule hiyo lakini ilipata taarifa kuwa mwalimu mkuu na naibu wake walikuwa nje ya shule.
Ripoti ya Mark Wachira – Kaunti ya Murang'a.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIBxf49mrpqkmaLCboGMpqyrmZ6crm7DwKarsJmenK5uusBmoq6lpaq6qsbAZqSwmZ6Ws7a62aJkrJmjlnqvtYyknKyhXp3Brrg%3D